EU kuipatia silaha jeshi la Ukraine zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 450
2022-02-28 14:08:52| CRI

Ofisa mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Josep Borrell amesema, nchi 27 wanachama wa Umoja huo wameamua kutoa silaha zenye thamani ya EURO milioni 450 na kuipatia jeshi la Ukraine, pamoja na mafuta na vifaa vya kujilinda vyenye thamani ya EURO milioni 50.

Borrell amesema mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuidhinisha hatua za vikwazo zitakazochukuliwa dhidi ya Russia, na mipango ya kuipatia misaada Ukraine kabla ya Jumatatu.