Baraza la Usalama la UM kufanya mkutano kuhusu hali ya Ukraine
2022-02-28 14:09:49| CRI

Baraza la Usalama la UM kufanya mkutano kuhusu hali ya Ukraine_fororder_3

Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama litaitisha tena Mkutano wa wazi kuhusu hali ya Ukraine. Imefahamika kuwa, mkutano huo ulioanzishwa na baadhi ya nchi za magharibi unalenga kujadili hali ya ubinadamu nchini Ukraine.

Kabla ya hapo, Baraza la Usalama lilifanya mkutano na kupitisha azimio No. 2623 ambalo lilitolewa na nchi kadhaa ikiwemo Marekani kuhusu kuitisha mkutano wa dharura wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Ukraine. Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun alihudhuria mkutano huo na hakupiga kura, ambapo alitoa ufafanuzi kuhusu msimamo wa China, akisema hivi sasa hali ya Ukraine inabadilika kwa kasi, na kazi kuu kwa sasa ni kwamba pande zote ziendelee kujizuia, ili kuepusha hali ya nchi hiyo kuzidi kuwa mbaya. Pia amesisitiza kuwa China inaunga mkono na kuhamasisha juhudi zote za kidiplomasia zinazochangia ufumbuzi wa amani wa mgogoro wa Ukraine, na kukaribisha Russia na Ukraine zifanye mazungumzo mapema. Pia China inaunga mkono Ulaya na Russia kufanya mazungumzo yenye usawa kuhusu suala la usalama la Ulaya, kushikilia wazo la usalama, na kuunda utaratibu wa usalama wa Ulaya wenye uwiano, ufanisi na uendelevu.