China yataoa ripoti kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Marekani
2022-03-01 09:29:48| cri

Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China imetoa ripoti kuhusu ukiukaji wa hali za binadamu nchini Marekani kwa mwaka 2021.

Ripoti hiyo inasema hali ya haki za binadamu nchini Marekani ambayo imekuwa na rekodi sugu, iliendelea kuwa mbaya katika mwaka 2021. Upotoshaji wa kisiasa ulifanya vifo kutokana na COVID-19 viwe vingi na kufanya nchi hiyo iwe na rekodi kubwa ya vifo.
Demokrasia feki ambayo imepuuza haki za kisasa na utekelezaji wa sheria wa kikatili vimefanya maisha ya wahamiaji na wakimbizi nchini Marekani yawe magumu. Ripoti hiyo pia imeonesha kuongezeka kwa vitendo vya ubaguzi dhidi ya watu wachache, hasa wenye asili ya Asia. Ripoti pia imesema vitendo vya upande mmoja vya Marekani vimezusha msukosuko mpya wa kibinadamu kote duniani.