China yatoa ripoti juu ya ukiukaji wa haki za binadamu wa Marekani
2022-03-01 10:31:31| CRI

China yatoa ripoti juu ya ukiukaji wa haki za binadamu wa Marekani_fororder_4

Ofisi ya habari ya Baraza la serikali ya China jana ilitoa ripoti juu ya ukiukaji wa haki za binadamu wa Marekani katika mwaka 2021.

Ripoti hiyo imesema hali ya haki za binadamu yenye sifa mbaya nchini Marekani imekuwa mbaya zaidi katika mwaka jana. Mchezo wake wa kisiasa umesababisha ongezeko la kasi la idadi ya watu wanaokufa kwa virusi vya Corona, na idadi ya vifo vinavyotokana na ufyatuaji risasi pia imeweka rekodi mpya nchini humo. Demokrasia feki inavuruga haki za kisiasa za watu, na utekelezaji wa sheria kimabavu umeyafanya maisha ya wahamiaji na wakimbizi yawe magumu zaidi nchini Marekani.

Ripoti hiyo pia imesisitiza hali mbaya zaidi ya ubaguzi wa Marekani dhidi ya watu wa makabila madogo, hasa wale wenye asili ya Asia. Ripoti hiyo inaongeza kuwa utendaji wa Marekani wa upande mmoja umesababisha msukosuko mpya wa kibinadamu kote duniani.