Duru ijayo ya mazungumzo ya amani ya Russia na Ukraine kufanyika kwenye mpaka wa Belarus na Poland
2022-03-01 10:38:03| CRI

Shirika la habari la Russia RIA Novosti limeripoti kuwa duru ijayo ya mazungumzo ya amani kati ya Russia na Ukraine itafanyika kwenye mpaka wa Belarus na Poland katika siku zijazo. Hayo ni kulingana na Vladimir Medinsky, mkuu wa ujumbe wa Russia katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Belarus.

Baada ya mazungumzo hayo Medinsky amesema kuwa cha muhimu zaidi ni kuwa walikubaliana kuendelea na mchakato wa mazungumzo, na kuongeza kuwa kila mjumbe sasa atarejea katika mji mkuu wa nchi yao ili kujadili zaidi misimamo yote ya mazungumzo na watakutana kwa duru inayofuata ya mazungumzo.

Amesema wamepata maswala kadhaa ambayo wanaweza kutabiri kwamba kutakuwa na misimamo ya pamoja.