SADC yazindua kituo cha kupambana na ugaidi cha kikanda nchini Tanzania
2022-03-01 10:32:23| CRI

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Jumatatu ilizindua kituo chake cha kupambana na ugaidi jijini Dar es Salaam Tanzania.

Kituo hicho kinalenga kuimarisha ushirikiano na nia ya nchi wanachama 16 wa SADC katika kukabiliana na changamoto za kiusalama, hasa tishio la ugaidi na itikadi kali katika kanda hiyo. Katibu mtendaji wa SADC, Elias Magosi amesema majukumu ya kituo hicho ni pamoja na kuishauri SADC juu ya kupambana na ugaidi na kuzuia sera za itikadi kali, kuweka programu na kusambaza maafisa ndani ya kanda hiyo. Pia kituo hicho kitakuwa na kazi ya kufanya utafiti, tathmini, uchambuzi na kusambaza taarifa kwa wakati kwenye mashirika ya kitaifa ya kupambana na ugaidi na kuzuia itikadi kali pamoja na wadau wengine husika, wakiwemo Umoja wa Afrika na washirika wa kimataifa.