Putin asema masuala yote yanayohusu usalama lazima yatiliwe maanani kwenye makubaliano na Ukraine
2022-03-01 10:33:16| CRI

Putin asema masuala yote yanayohusu usalama lazima yatiliwe maanani kwenye makubaliano na Ukraine_fororder_5

Ikulu ya Russia imetoa taarifa ikisema rais wa Russia Vladmir Putin amesema masuala yote yanayohusu usalama lazima yatiliwe maanani kwenye makubaliano na Ukraine.

Akiongea kwa simu na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, Putin amesema makubaliano yatawezekana tu endapo wasiwasi wa usalama wa Russia utazingatiwa ikiwemo mamlaka ya Russia juu ya Crimea, pamoja na dhamira ya nchi ya kutatua kazi za kuondoa majeshi na unazi za Ukraine, na suala la hadhi ya nchi kutopendelea upande wowote. Putin amesisitza kuwa Russia iko tayari kwa mazungumzo na Ukraine na kueleza matumaini yake kwamba mazungumzo hayo yatakuwa na matokeo ya kuridhisha.

Kwa upande wa ikulu ya Ufaransa imesema Macron ameitaka Russia kuheshimu sheria ya kimataifa na kulinda raia wa kawaida, pamoja na kuthibitisha ulazima wa kuweka silaha chini mara moja.