Ukraine yasema shambulizi la Russia dhidi ya mnara wa TV wa Kiev lasababisha vifo vya watu watano
2022-03-02 09:48:27| CRI

Ukraine yasema shambulizi la Russia dhidi ya mnara wa TV wa Kiev yasababisha vifo vya watu watano_fororder_3

Idara ya utoaji wa huduma za dharura ya Ukraine imesema kwenye Facebook kuwa, watu watano wameuawa na wengine zaidi ya watano kujeruhiwa katika shambulizi la Russia dhidi ya mnara wa TV wa Kiev.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine imesema hapo awali kuwa uendeshaji wa vituo vya televisheni utakatizwa kutokana na mashambulizi hayo.