Sudan Kusini, Benki ya Dunia na UNICEF wazindua kampeni ya kuongeza uelewa wa afya kwa watu
2022-03-02 09:46:56| CRI

Wizara ya Afya ya Sudan Kusini, Benki ya Dunia na UNICEF jana Jumanne walizindua kampeni ya mawasiliano ili kuangazia programu ya pamoja ya afya na kuongeza uelewa miongoni mwa muungano mpana wa washirika, kwa lengo la kuongeza uwekezaji katika sekta ya afya.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na UNICEF mjini Juba, kampeni hiyo ya mawasiliano itakayofanyika katika mwezi mzima wa Machi na kwenye majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari, ikitoa ujumbe wa huduma za pamoja za afya, itashirikisha mabango ya matangazo, video na matangazo ya huduma za umma, ambapo yataangazia umuhimu wa hatua mbalimbali za afya, zikiwemo kampeni za kinga na chanjo dhidi ya COVID-19.