China yaimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini katika kuhimiza maendeleo ya kilimo
2022-03-03 09:59:14| CRI

China yaimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini katika kuhimiza maendeleo ya kilimo_fororder_5

Waziri wa kilimo na mambo ya vijiji wa China Bw. Tang Renjian amesema China itaimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini kwa kushirikiana na pande zote na kuhimiza maendeleo endelevu ya kilimo na maeneo ya vijiji chini ya pendekezo la maendeleo ya dunia.

Tang alisema hayo aliposhiriki kwenye shughuli ya kimataifa ya ngazi ya juu iitwayo “Kuimarisha Ushirikiano wa Kusini na Kusini na wa Pande tatu kwa ajili ya Maendeleo ya kilimo ya dunia”, ambayo ilifanyika Jumatatu, ikiandaliwa na Wizara ya kilimo na mambo ya vijiji ya China na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Akihutubia ufunguzi, Mkurugenzi mkuu wa shirika la FAO Bw. Qu Dongyu amesema Ushirikiano wa Kusini na Kusini na wa Pande tatu ni moja ya njia muhimu za kukabiliana na changamoto zinazotokana na njaa, utapiamlo, umaskini na kukosekana kwa usawa duniani.

Tang Renjian amesema China inatarajia kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na shirika la FAO na wenzi wengine, na kutoa mchango katika kupambana na njaa na kupunguza umaskini.