Marekani yanyakua pesa za Waafghanistan ikitetea haki duniani
2022-03-03 14:27:32| cri

Marekani yanyakua pesa za Waafghanistan ikitetea haki duniani_fororder_VCG111369370104

Rais Joe Biden wa Marekani hivi majuzi alitia saini amri ya rais kuhusu fedha iliyogandishwa ya Benki Kuu ya Afghanistan nchini Marekani, na kutangaza kuwa fedha hizo za dola bilioni 7 za Kimarekani zitagawanywa katika sehemu mbili: nusu moja itatumika kuwalipa fidia wahasiriwa wa tukio la Septemba 11, na nusu nyingine itatumika kwa ajili ya Waafghanistan kama msaada unaotolewa na Marekani.

Hili ni jambo la kuwashangaza watu, kwani ikiwa nchi tajiri zaidi duniani, Marekani ilinyakua fedha za Afghanistan ambayo ni moja ya nchi inayobaki nyuma kimaendeleo zaidi, na wananchi wake wanakabiliwa na njaa na taabu nyingine kubwa. Je, si wakati wote Marekani inadai inatetea haki na haki za binadamu duniani?

Kufuatia ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, hivi sasa Afghanistan inakabiliwa na kile ambacho kinaweza kuwa janga kubwa zaidi la kibinadamu duniani. Vita iliyoanzishwa na Marekani na kuendelea kwa zaidi ya miaka 20 imeleta janga kubwa kwa Afghanistan, na ustawi wa watu wake umeharibiwa kabisa. Katika nusu ya kwanza ya mwaka jana, mapambano ya mwisho kati ya kundi la Taliban na jeshi la serikali ya zamani nchini humo yalivuruga uzalishaji wa nafaka wa majira ya kiangazi. Wakati huo huo Afghanistan imekuwa ikikabiliwa na ukame mkubwa katika miaka miwili iliyopita. Mambo hayo yameathiri kilimo, ambacho ndio nguzo kuu ya uchumi wa nchi hiyo. Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limeonya mwishoni mwa Oktoba mwaka 2021 kwamba, zaidi ya nusu ya Waafghanistan watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Zaidi ya hayo, sasa ni majira ya baridi kali, Waafghanistan wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme na uhaba mkubwa wa vifaa vya kukinga baridi. Wakati huo huo, juhudi za kukabiliana na janga la COVID-19 nchini humo pia zimevurugwa sana vizuizi vya kimataifa.

Kama mzushi wa taabu nchini Afghanistan, Marekani ilipuuza hali hizi mbaya na kuidhuru tena nchi hiyo Waafghanistan walihitaji msaada sana.

Kitendo hicho cha Marekani kimekasirisha sana Waafghanistan. Waandamanaji wamekusanyika katika mitaa ya Kabul, wakisema mali zilizonyakuliwa na Marekani ni za watu wa Afghanistan, na Marekani ilikuwa ni kama mwizi. Kuhusu Marekani kuchukua pesa hizi kuwafidia wahasiriwa wa tukio la Septemba 11, waandamanaji wamesema Marekani inapaswa kutoa fidia kwa Waafghanistan zaidi ya 240,000 waliopoteza maisha katika vita vya Afghanistan iliyoendelea kwa miaka 20.

Marekani inadai kuwa “mtetezi” wa haki na haki za binadamu duniani, lakini kunyakua fedha za Waafghanistan kumethibitisha tena kuwa kwa kweli Marekani ni mkiukaji wa haki na haki za binadamu duniani.