China yatoa waraka kuhusu maendeleo ya michezo kwa watu wenye ulemavu
2022-03-03 19:05:06| cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka kuhusu kuendeleza michezo ya walemavu, ili kuhimiza juhudi za kuendeleza michezo ya walemavu nchini China. Waraka huo wenye kichwa “Michezo ya walemavu ya China: Maendeleo na Ulinzi wa Haki," umetolewa siku moja kabla ya ufunguzi wa Michezo ya walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022.

Tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, pamoja na kupiga hatua katika masuala ya watu wenye ulemavu, China pia imeendelea kuendeleza michezo ya walemavu, na kuwa na njia yenye umaalum wa China na inayoheshimu mwelekeo wa nyakati. Waraka huo umebainisha kuwa maendeleo ya kihistoria yamepatikana katika sekta ya michezo tangu mkutano wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China wa mwaka 2012.

Waraka pia unasema China inazingatia shughuli za urekebishaji na mazoezi ya mwili kwa watu wenye ulemavu kama moja ya vipengele muhimu katika kutekeleza mikakati yake ya kitaifa ya afya kwa wote, na kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu katika sekta ya michezo.

Waraka huo pia unasema China imetoa mchango mkubwa kwenye mambo ya michezo ya walemavu kimataifa, inajishughulisha kikamilifu na masuala ya michezo ya kimataifa kwa walemavu. na inaendelea kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa ya watu wenye ulemavu, kujenga urafiki kati ya watu wa nchi zote, ikiwa ni pamoja na wale wenye ulemavu.

Waraka huo pia umesema michezo ya walemavu ni mfano wazi wa maendeleo na maendeleo ya haki za binadamu nchini China, na michezo hiyo pia inaendeleza maadili ya pamoja ya ubinadamu, kuhimiza mawasiliano, maelewano na urafiki kati ya watu duniani kote, na kuchangia busara za China katika kujenga usimamizi wa dunia ulio wa haki, na shirikishi kwenye mambo ya haki za binadamu, na kudumisha amani na maendeleo duniani.