Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China kufunguliwa Ijumaa mjini Beijing
2022-03-03 16:06:29| cri

 

Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China utafunguliwa ijumaa saa tisa alasiri katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, na utafanyika kwa siku sita kabla ya kufungwa Machi 10.

Ajenda kuu ya mkutano huo ni kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi za halmashauri ya kudumu ya baraza hilo, na ripoti ya miswada iliyowasilishwa na wajumbe kwa baraza hilo; kuhudhuria Mkutano wa tano wa Bunge la 13 la Umma la China, kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi za serikali na ripoti nyingine husika; na kujadili na kupitisha maazimio na ripoti, ikiwemo Azimio la Kisiasa la Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China.