Nchi za Afrika zashiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi
2022-03-03 14:26:03| cri

Nchi za Afrika zashiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi_fororder_2

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi inayoendelea imevutia macho ya dunia. Jumla ya nchi tano za Afrika, ambazo ni Kenya, Nigeria, Madagascar, Morocco na Eritrea zimeshiriki kwenye michezo hiyo. Kwa nchi za Afrika, kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, sio tu ni ishara ya ujasiri wa kukabiliana na changamoto, bali pia kunaonesha nia ya bara hiyo ya kuelekea siku zijazo.

Kutokana na mazingira ya kiasili na hali ya uchumi, ni nchi 15 tu za Afrika ambazo zimeshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Kutokana na ukosefu wa barafu na theluji, wanamichezo wa michezo ya barafu na theluji barani Afrika wanakabiliwa na changamoto kubwa katika mazoezi yao ya siku za kawaida. Licha ya watu wachache kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi nje ya nchi, wachezaji wengine wengi wanaweza tu kutafuta njia mbadala kujiandaa na mashindano. Kwa mfano, wanamichezo wa kuteleza kwenye barafu wa Ethiopia wanafanya mazoezi barabarani, na wachezaji nchini Morocco wanafanya mazoezi jangwani ili kujiandaa na mashindano ya kutekeleza theluji. Hata hivyo, hali hiyo ngumu haikuwavunja moyo wanamichezo wa Afrika. Mchezaji wa bobsleigh wa Ghana Bw. Frimpong, ambaye ameshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, huwa anakimbia na kunyanyua uzito ili kujiandaa na mashindano, na anasema, kamwe changamoto hiyo haitamzuia.

Mambo haya ya kutia moyo ya wanariadha hawa yanauthibitishia ulimwengu kwamba, Waafrika, ambao wengi wao hawajaona theluji na barafu, wanaweza kushindana kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Ingawa wanariadha wa Afrika bado hawajashinda medali zozote katika Olimpiki ya Majira ya Baridi, lakini shauku yao ya kushiriki kwenye michezo ya barafu na theluji imeleta msukumo mkubwa katika maendeleo ya michezo hiyo barani Afrika.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi imewapa Waafrika fursa ya kuelewa na kufurahia michezo ya barafu na theluji, na kuwafanya Waafrika wengi zaidi kupenda michezo hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya uchumi na jamii, nchi nyingi za Afrika zimejenga viwanja vya kuteleza kwenye theluji na barafu, na kuanzisha timu zaidi za michezo ya barafu na theluji. Kwa mfano, mwezi Oktoba mwaka jana, Kenya ilianzisha timu ya taifa ya Curling, na kuwa nchi ya pili barani Afrika kushiriki rasmi katika mchezo wa Curling. Wakati huo huo, serikali ya nchi hiyo ilianza kukuza mchezo huo shuleni, ili kushiriki katika michuano ya kimataifa ya vijana ya Curling. Kenya pia inajadili ushirikiano na China, Denmark na nchi nyingine zenye nguvu katika michezo ya Curling ili kuendeleza mchezo huo.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela alisema, “Tukiwa na ujasiri wa kukubaliana na changamoto katika maisha yetu, hata ndoto za ajabu zaidi zinaweza kutimia.” Kwa nchi za Afrika, kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kutachochea maendeleo ya michezo ya majira ya baridi na kuongeza imani yao katika kushinda changamoto yoyote.