Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa
2022-03-04 15:31:02| cri

Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa_fororder_src=http___inews.gtimg.com_newsapp_bt_0_14587476528_1000&refer=http___inews.gtimg

Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China umefunguliwa leo kwenye Ukumbi Mkuu wa Mikutano ya Umma wa China mjini Beijing. Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China akiwemo Rais Xi Jinping wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo. 

Karibu wajumbe 2,000 kutoka vyama mbalimbali, makabila mbalimbali na nyanja mbalimbali wamehudhuria mkutano huo wa siku 6, na watajadili ripoti iliyotolewa na kamati ya kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa kuhusu utekelezaji wa mapendekezo yao, na kusikiliza ripoti kuhusu kazi ya serikali.