Nafasi ya wanawake katika Siasa
2022-03-04 10:05:19| CRI

Mikutano miwili mikubwa ya kisiasa nchini China imeanza hapa Beijing, na katika mikutano hiyo wajumbe kutoka kada tofauti za maisha wanakutana na kutathimini kazi za serikali kwa mwaka uliopita na kupanga kazi za serikali kwa mwaka unaofuata. Wanawake nao hawako nyuma kwenye uwanja huu wa siasa, kwani wanashiriki kikamilifu katika kutunga na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yanayofikiwa katika mikutano hiyo. Katika kipindi chetu cha Ukumbi wa Wanawake hii leo, tutazungumzia zaidi nafasi ya wanawake katika siasa, na jinsi wanavyotumia nafasi zao kuwainua wawawake wenzao kiuchumi.