Rais Xi ahudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya olimpiki ya walemavu majira ya baridi ya Beijing 2022
2022-03-04 20:57:06| cri

Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 imefunguliwa rasmi leo hapa Beijing kwenye uwanja wa michezo wa Taifa wa Beijing, unaojulikana pia kama “Kiota”. Rais Xi Jinping wa China leo amehudhuria sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo.

Kuanzia leo Machi 4 hadi Machi 13, wanamichezo walemavu kutoka sehemu mbalimbali duniani watashindana katika matukio 78 katika michezo sita tofauti, 39 kwa wanaume, 35 kwa wanawake na mashindano manne mchanganyiko. Michezo itafanyika katika viwanja sita vilivyopo katika maeneo ya Beijing, Yanqing na Zhangjiakou.

Wanamichezo kutoka Israel, Azerbaijan na Puerto Rico ndio watakuwa wa kwanza kukutana kwenye michezo yao ya kwanza kwenye michezo hii.