Tanzania yakumbwa na matukio makali ya hali ya hewa mwaka 2021 kutokana na mabadiliko ya tabianchi
2022-03-04 10:29:06| CRI

Tanzania yakumbwa na matukio makali ya hali ya hewa mwaka 2021 kutokana na mabadiliko ya tabianchi_fororder_4

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) jana ilisema katika mwaka 2021 Tanzania ilikumbwa na matukio makali ya hali ya hewa yaliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na mvua kubwa, mafuriko, ukame wa muda mrefu, upepo mkali, na joto kali.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo juu ya hali ya hewa ya Tanzania katika mwaka 2021 imesema matukio hayo makali yanatishia sana maisha ya watu.

Taarifa hiyo imesema mvua kubwa zilinyesha mwezi Januari na Februari mwaka jana, na kusababisha mafuriko kwenye baadhi ya maeneo nchini humo, hasa kwenye mikoa ya kusini na magharibi, ambapo miundombinu, makazi na mashamba yaliharibiwa vibaya. Na mwezi Novemba mwaka jana ulikuwa kipindi chenye joto kali zaidi, na kiwango cha joto kali katika mwezi Disemba mwaka jana kimekuwa nafasi ya tatu tangu mwaka 1970. Pia baadhi ya maeneo yalikumbwa na ukame hasa kwenye msimu wa mvua kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka jana.