Mambo 10 yako kwenye ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China
2022-03-04 14:53:06| cri

Mambo 10 yako kwenye ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China_fororder_图像_2022-03-04_145605

Msemaji wa mkutano wa bunge la umma la China Bw. Zhang Yesui, amesema Bunge la Umma la China litafungua mkutano wake wa kila mwaka Jumamosi asubuhi hapa Beijing, na mkutano huo utafungwa tarehe 11 Machi.

Bw. Zhang amesema ajenda ya kikao cha tano cha Bunge la 13 la Umma imepitishwa Ijumaa asubuhi ikiwa na vipengele 10. Bw. Zhang pia amesema wajumbe wa mkutano huo watapitia nyaraka mbalimbali ikiwa ni pamoja na ripoti ya kazi ya serikali na kujadili rasimu ya marekebisho ya kanuni za Bunge, na mabaraza ya umma ya mitaa na serikali za mitaa.

Pia watajadili rasimu ya uamuzi kuhusu idadi ya wajumbe wa bunge la 14 na namna ya kuwachagua, na rasimu za mbinu mbili kuwachagua wajumbe kutoka mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Macao.