Ripoti ya kazi ya serikali ya China: soko kubwa la wazi litatoa fursa zaidi kwa makampuni kutoka duniani kote
2022-03-05 10:31:41| cri

Ripoti ya kazi ya serikali ya China kwa mwaka 2022 iliyowasilishwa kwenye Bunge la Umma la China tarehe 5, imeeleza kutumia kikamilifu mitaji ya kigeni, na kufungua soko kubwa la China, jambo ambalo hakika litatoa fursa zaidi kwa makampuni kutoka nchi zote kujiendeleza nchini China.

 

Ripoti hiyo imeeleza kuwa ni muhimu kupanua maeneo yanayoruhusiwa kuwekezwa na nchi za nje, na kuunga mkono mitaji ya kigeni kuwekezwa katika sera za uzalishaji wa hali ya juu na kati, utafiti na maendeleo, huduma za kisasa, na vile vile katika mikoa ya kati magharibi, na kaskazini mashariki.

 

Ripoti pia imesisitiza kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na nchi nyingine duniani ili kupata maendeleo kwa pamoja.