Ripoti ya kazi ya serikali ya China: kupinga vikali vitendo vya ufarakanishaji vya “watu wanaotaka kuifanya Taiwan ijitenge na China" na uingiliaji kutoka nje
2022-03-05 10:37:08| cri

Ripoti ya kazi ya serikali ya China iliyotolewa tarehe 5 imeeleza kuwa China inapinga kithabiti vitendo vya ufarakanishaji vinavyofanywa na "makundi ya watu wanaotaka kuifanya  Taiwan ijitenge na China" na vitendo vya uingiliaji kutoka nje.

 

Ripoti ya kazi ya serikali imesema ni muhimu kuzingatia sera na kanuni kuu za kazi kuhusu suala la Taiwan, kutekeleza mkakati wa jumla wa Chama cha kutatua suala la Taiwan katika  zama mpya, kuzingatia sera ya kuwepo kwa China Moja na "Makubaliano ya 1992", na kuhimiza maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya China bara na Taiwan na kutimiza muungano wa taifa.

 

Ripoti ya kazi ya serikali imeeleza kuwa watu wa pande zote mbili za Mlangobahari wa Taiwan wanapaswa kufanya kazi pamoja na kutimiza ustawi wa wachina wote.