Ripoti ya Kazi ya Serikali ya China yasisitiza kupambana vikali na uhalifu wa utekaji nyara na usafirishaji haramu wa wanawake na watoto
2022-03-05 10:35:04| cri

Ripoti ya kazi ya serikali ya China iliyotolewa tarehe 5 mjini Beijing imeeleza kuwa ni muhimu kupambana vikali na uhalifu wa usafirishaji haramu wa wanawake na watoto, na kulinda kwa uthabiti haki na maslahi halali ya wanawake na watoto.

 

Ripoti ya kazi ya serikali pia imesema ni muhimu kuhakikisha watu wanaishi na kufanya kazi kwa amani na katika mazingira ya kuridhika, na kukuza utulivu na utulivu wa kijamii. Ripoti pia imehimiza ubunifu na kuboresha uwezo wa utawala wa kijamii wa ngazi ya shina. Ripoti pia imetaka kuendeleza kazi ya kijamii na kusaidia maendeleo ya mashirika ya kijamii, misaada ya kibinadamu, huduma za kujitolea, na ustawi wa umma.

 

Ripoti hiyo pia imesisitiza kwamba serikali katika ngazi zote na watumishi wake lazima wazingatie usalama wa watu, kuangalia ukweli, kufanya kazi kivitendo, kutafuta matokeo kivitendo, kuitikia matatizo ya watu kwa wakati, na kushughulikia kwa uthabiti vitendo vya kutowajibika vinavyopuuza haki halali na maslahi ya watu.