Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China waanza Beijing
2022-03-05 10:28:03| cri

Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China waanza Beijing_fororder_VCG111371860070

 

Mkutano wa Tano wa Bunge la 13 la Umma la China umeanza leo tarehe 5 mjini Beijing, na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali pamoja na karibu wajumbe 3,000 wa Bunge la Umma.

 

Kwa mujibu wa ajenda, mkutano huo utapitia ripoti ya kazi ya serikali kuu, na kufafanua malengo na majukumu makuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China kwa mwaka huu na mkakati wa utawala nchi wa serikali. Ripoti ya mpango inayohusiana na uchumi wa taifa na maisha ya watu na ripoti ya bajeti, ambayo inachukuliwa kuwa kitabu cha hesabu cha kitaifa, pia iliwasilishwa katika ufunguzi wa mkutano huo kwa ajili ya kupitiwa.

 

Katika nusu ya pili ya mwaka 2022, Chama cha Kikomunisti cha China kitafanya mkutano wake mkuu wa 20 ili kufanya majumuisho ya kazi za miaka mitano iliyopita, na kuweka mpango wa maendeleo kwa siku zijazo. Kwenye mkutano huo ufuatiliaji utakuwa jinsi China, ambayo imeanza safari mpya ya kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, itakavyoendeleza uchumi na jamii.