Rais Xi Jinping atembelea wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China na kushiriki kwenye mjadala wa wajumbe wa mkoa wa Mongolia ya Ndani
2022-03-06 17:19:29| Cri

Rais Xi Jinping wa China leo mchana amewatembelea wajumbe kutoka sekta za kilimo na utoaji wa huduma za jamii wanaoshiriki katika Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China.

Pia rais Xi ameshiriki katika kikao cha pamoja cha kikundi cha wajumbe hao, na kusikiliza maoni na mapendekezo yao. 

Na rais Xi ameshiriki kushiriki kwenye mjadala wa wajumbe wa mkoa wa Mongolia ya Ndani.