China na Marekani zatakiwa kuhimiza uhusiano kati yao kurejea katika njia sahihi yenye utulivu
2022-03-07 17:17:11| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ameeleza kuwa China na Marekani zinatakiwa kurejesha moyo wa kuondoa mikwaruzano, na kujitayarisha kufunga safari mpya.

Wang Yi amesema, China inaona kuwa ushindani kati ya nchi kubwa si maudhui ya zama hii. Wakati wa utandawazi wa dunia ambao nchi zote zinajiendeleza kwa kutegemeana, vile China na Marekani zinavyotafuta njia sahihi ya kutendeana zikiwa nchi kubwa, ni suala ambalo halijawahi kukabili jamii ya binadamu, vilevile ni suala litakalotatuliwa kwa juhudi za pamoja za nchi hizo mbili.

Wang amesisitiza kuwa huu ni mwaka wa 50 tangu kutolewa kwa “Taarifa ya Shanghai”. Katika siku zilizopita China na Marekani zilitumia ushirikiano kuchukua nafasi ya kukabiliana na kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili, na kuhimiza amani na ustawi wa dunia. Katika siku za baadae, pande hizo mbili zinatakiwa kuhimiza sera za Marekani kwa China kurejea katika njia sahihi inayofuata wazo la kimantiki, ili kuufanya uhusiano kati ya pande hizo mbili urejee kwenye njia sahihi yenye utulivu.