Wang Yi asisitiza kufanya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kuwa "Ukanda wa Maendeleo" na "Njia ya Furaha"
2022-03-07 17:48:58| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi leo amesema kuwa licha ya athari za janga la COVID-19 na mambo mengine, ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" bado unashikilia kasi nzuri.

Wang Yi alifahamisha kuwa tangu mwaka 2021, nchi nyingine 10 zimesaini nyaraka za ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na China, na idadi ya wanachama wa familia ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imefikia 180. China imeshirikiana na nchi 20 zinazoendelea katika uzalishaji wa pamoja wa chanjo, ambazo nyingi zinalenga nchi zilizo kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Idadi ya washirika katika ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" inaendelea kupanuka, msingi wa ushirikiano unazidi kuwa imara, na matarajio ya ushirikiano ni mapana zaidi, ambayo bila shaka yatafungua matarajio mapya ya maendeleo duniani baada ya kipindi janga la Corona.

Aidha Wang Yi amesema katika siku zijazo, China itashirikiana na jamii ya kimataifa kuendelea kuhimiza ujenzi wa pamoja wa hali ya juu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kujitahidi kufikia ushirikiano wa viwango vya juu, ufanisi wa juu wa uwekezaji, usambazaji wenye ubora wa juu na ustahimilivu wa juu wa maendeleo. "Ukanda Mmoja, Njia Moja" itajengwa kuwa "Ukanda wa Maendeleo" ambao utanufaisha dunia na "Njia ya Furaha" ambayo itanufaisha watu wa nchi zote.