Wang Yi: ni lazima kuzuia kutokea mzozo mkubwa wa kibinadamu nchini Ukraine
2022-03-07 17:27:23| cri

Mjumbe wa Baraza la Taifa la China na Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Wang Yi amesisitiza ulazima wa kuzuia kutokea kwa mzozo mkubwa wa kibinadamu nchini Ukraine, na kwamba China iko tayari kutoa mapendekezo sita juu ya hili.

Wang alisema, kwanza, operesheni za kibinadamu lazima zizingatie kanuni za kutopendelea na haki, na kutoingiza siasa kwenye masuala ya kibinadamu; pili, kufuatilia kikamilifu watu waliokimbia makazi yao nchini Ukraine na kuwashughulikia ipasavyo; tatu, kulinda raia ipasavyo, na kuzuia kutokea kwa matatizo yatakayofuata ya kibinadamu nchini Ukrainia. Nne ni kuhakikisha shughuli za misaada ya kibinadamu zinaendelea vizuri na salama, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za kibinadamu za haraka, salama na bila vikwazo; tano ni kuhakikisha usalama wa raia wa kigeni nchini Ukraine na kuwaruhusu waondoke Ukraine kwa usalama na kutoa msaada wakati wakiondoka. Sita, kuunga mkono Umoja wa Mataifa kutekeleza jukumu la kuratibu katika usaidizi wa kibinadamu nchini Ukraine, na kuunga mkono kazi ya mratibu wa mzozo wa Ukraine wa Umoja wa Mataifa.

Wang alitangaza kuwa, China inapenda kuendelea na juhudi zake ili kukabiliana na janga la kibinadamu. Chama cha Msalaba Mwekundu cha China kitatoa misaada ya dharura ya kibinadamu kwa Ukraine haraka iwezekanavyo.