Nchi zote zatakiwa kuwa na mshikamano katika mwaka 2022 unaokabiliwa na changamoto mbalimbali
2022-03-07 17:11:22| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesisitiza kuwa China ikiwa nchi kubwa inayowajibika, itaendelea kushikilia utaratibu wa pande nyingi, kushirikiana na nchi zote zinazopenda amani na kutafuta maendeleo kwa pamoja, kuimarisha umoja na ushirikiano, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, na kuendelea kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja, ili kujenga mustakabali mzuri zaidi kwa dunia.

Wang Yi amesema hayo kwenye Mkutano wa Tano wa Bunge la 13 la Umma la China. Amesema huu vilevile ni mwaka utakaokabiliwa na changamoto mbalimbali. Janga COVID 19 bado linaendelea, huku mgogoro wa Ukraine ukiibuka, hali ambayo imeongeza sintofahamu ya hali ya kimataifa. Katika kipindi hiki muhimu, kinachohitajika na nchi zote ni bora kuwa na mshikamano badala ya ufarakanishaji, na ni bora kuwa na mazungumzo badala ya mvutano.

Wang alipozungumzia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, amesisitiza mafanikio ya michezo hiyo si kama tu ni ya sekta ya michezo, bali ni mafanikio ya mshikamano.