Wang Yi asema uhusiano kati ya China na Russia hautaingiliwa na kuchochewa na upande wa tatu
2022-03-07 17:09:24| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi leo amesema kuwa uhusiano kati ya China na Russia una thamani ya uhuru na kujitegemea.

Amefafanunua kuwa China na Russia ni majirani muhimu na wa karibu zaidi na washirika wa kimkakati , na kusema uhusiano wa pande mbili kati ya China na Russia ni moja ya uhusiano muhimu zaidi duniani. Ushirikiano wa pande hizi mbili sio tu unaleta tija na ustawi wa watu wa pande mbili, bali pia unachangia amani, utulivu na maendeleo duniani.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa hivi karibuni na pande hizo mbili, imeonesha wazi kwa dunia kwamba China na Russia wanapinga kwa pamoja kurejea kwa mawazo ya vita baridi, kupinga kuchochea makabiliano ya kiitikadi, kutetea uimarishaji wa demokrasia ya mahusiano ya kimataifa, na kudumisha madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa.