Wang Yi: kujiona ni wewe tu sio maana ya demokrasia, bali ni maafa ya demokrasia
2022-03-07 17:52:04| cri

Mjumbe wa Baraza la Taifa la China na Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Wang Yi amesema leo tarehe 7 kuwa, mwaka 2021, Marekani ilifanya kile kinachoitwa "mkutano wa kilele wa demokrasia" chini ya mwavuli wa "demokrasia", ikiondoa karibu nusu ya nchi zote za dunia, na kuchora mstari kwa mujibu itikadi tofauti, na kuzusha mfarakano duniani, kitendo ambacho tayari kimevuruga moyo wa demokrasia, na kufanya tena mkutano kama huo halitakuwa jambo la kuheshimiwa.

Wang Yi ameeleza kuwa demokrasia ya umma katika mchakato mzima wa China ni demokrasia pana, halisi na yenye ufanisi, ambayo imeungwa mkono kwa moyo wote na watu wa China. China inaamini kwamba kufafanua "viwango vya kidemokrasia" kulingana na mtindo wa Marekani ni udhihirisho wa kutokuwa na demokrasia. Kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa jina la "demokrasia" kunaweza tu kuleta maafa kwa watu. Kujiona ni wewe tu sio maana ya demokrasia, bali ni maafa ya demokrasia.