Wang Yi: "Mkakati wa Eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki" kwa hakika utashindwa
2022-03-07 17:39:17| cri

Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Wang Yi leo tarehe 7 amesema “Mkakati wa Eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki” (Indo-Pacific Strategy) wa Marekani ni mkondo unaokwenda kinyume na maono ya pamoja ya nchi za kanda hiyo ya kutafuta amani, maendeleo, ushirikiano na mafanikio ya pamoja, kwa hivyo kwa hakika hauna mustakbali.

 

Wang Yi ameeleza kuwa kile kinachoitwa “Mkakati wa Eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki” wa Marekani umekuwa sawa na siasa ya kikundi. Kinacholeta si baraka, bali utaharibu amani na utulivu wa kikanda. Kusudi lake halisi ni kujaribu kuunda toleo la NATO katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki, ni kudumisha mfumo wa umwamba unaotawaliwa na Marekani, kuathiri muundo wa ushirikiano wa kikanda kwenye kitovu cha ASEAN, na kuharibu maslahi ya jumla na ya muda mrefu ya nchi za kikanda.

 

Wang Yi alisisitiza kuwa China siku zote imejikita katika eneo la Asia na Pasifiki, ikijenga Asia na Pasifiki, na kunufaisha Asia na Pasifiki. Inakaribisha mapendekezo ambayo yanakidhi hali halisi ya kanda na mahitaji ya wahusika wote, na inapinga kwa uthabiti mapendekezo ya kuzua migogoro ya kikanda na kuunda makabiliano ya kundi moja moja. Amesema China inapenda kushirikiana na pande zote kutofautisha usahihi na kosa, kufuata njia sahihi, kupinga kuzuka kwa “kundi dogo” la makabiliano katika eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki, kujenga "jukwaa kubwa" la ushirikiano wa Asia na Pasifiki, na kuungana mkono kuelekea jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja.