Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa upatikanaji wa bidhaa za kilimo, na kujenga mfumo madhubuti wa uhakikisho wa kijamii
2022-03-07 08:43:28| CRI

Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa upatikanaji wa bidhaa za kilimo, na kujenga mfumo madhubuti wa uhakikisho wa kijamii_fororder_1128443977_16465777051181n

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ipasavyo kuboresha uwezo wa uzalishaji wa kilimo, na kuendelea na juhudi za kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya uhakikisho wa kijamii.

Rais Xi amesema hayo alipokutana na washauri wa kisiasa wa taifa kutoka sekta za kilimo na uhakikisho wa kijamii, walioko mjini Beijing kuhudhuria mkutano wa Baraza la mashauriano ya kisasa la China (CPPCC).

Rais Xi ameshiriki kwenye mijadala ya wajumbe wa sekta hizo, ambapo alisikiliza maoni na mapendekezo yao. Rais Xi amesisitiza muhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa mazao muhimu ya kilimo, hasa nafaka, kuwa ni kipaumbele katika kuendeleza vijiji.

Rais Xi kwa niaba ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China pia ametoa salamu za kila la heri za siku ya kimataifa ya wanawake, kwa wanawake wa makabila yote.