Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi leo kwenye mkutano na wanahabari amezungumzia uhusiano kati ya China na Afrika akisema kwamba mawaziri wa mambo ya nje wa China kila mwaka kwanza wanatembelea Afrika, kitendo ambacho kinaonesha uungaji mkono imara wa China kwa maendeleo na ufufukaji wa Afrika.
Bw. Wang amesema kwa miaka mingi, China imejenga zaidi ya kilomita 10,000 za reli, karibu kilomita laki moja za barabara, karibu bandari 100, na hospitali na shule zisizo na idadi barani Afrika, na kusisitiza kwamba huu sio “mtego wa madeni”, bali ni alama za ushirikiano.
Wang amebainisha kuwa mwaka uliopita ulikuwa mwaka mzuri kwa ushirikiano wa China na Afrika, kwani pande mbili zilifanya kwa mafanikio mkutano wa 8 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ambapo rais Xi Jinping alitangaza miradi tisa ya ushirikiano na Afrika, kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya pamoja ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja katika enzi mpya, na kuongeza msukumo mpya katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika.
Aidha amesema China itahimiza kwa nguvu moyo wa Ushirikiano na Urafiki kati ya China na Afrika na kushirikiana na nchi za Afrika huku ikizingatia kazi tatu: kwanza kuhimiza kwa nguvu ushirikiano na Afrika katika mapambano dhidi ya janga la Corona, pili kuhimiza maboresho na kupandisha ngazi ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika, na tatu kuhimiza wazo la Maendeleo ya Amani katika Pembe ya Afrika.