Nchi takriban mia moja zaunga mkono pendekezo la maendeleo ya dunia
2022-03-07 17:19:39| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema, pendekezo alilotoa rais Xi Jinping kuhusu maendeleo ya dunia linalingana na mahitaji ya pande zote, ambalo limeungwa mkono haraka na Umoja wa Mataifa pamoja na nchi karibu mia moja. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi zote kutekeleza vizuri pendekezo hili muhimu, na kutoiacha nyuma nchi yoyote, ili kujenga kwa pamoja Jumuiya ya Maendeleo ya Pamoja ya Dunia.

Wang Yi ameeleza kuwa nadharia kuu ya Pendekezo la Maendeleo ya Pamoja linatanguliza maslahi ya wananchi, ambalo lengo kuu ni kuchangia utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030. 

Wang pia amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na pande zote, kuangazia masuala makuu yanayozikabili nchi zinazoendelea zikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini, usalama wa chakula, ufufuaji wa uchumi, ajira na mafunzo, elimu na afya, na maendeleo ya kijani, na kuchangia katika kutimiza malengo 17 ya maendeleo endelevu mwaka 2030.