Xi Jinping aitisha mkutano kwa njia ya video na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani
2022-03-08 20:07:49| Cri

Rais Xi Jinping wa China leo mchana wa tarehe 8 ameitisha mkutano kwa njia ya video akiwa na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz hapa Beijing.

Katika mazungumzo yao rais Xi alisisitiza kuwa hali ya Ukraine inatia wasiwasi, na China inasikitishwa na kurejesha tena vita katika bara la Ulaya. Amesema China inashikilia kwamba mamlaka na ukamilifu wa ardhi kwa nchi zote yanapaswa kuheshimiwa, madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa lazima zifuatwe, wasiwasi halali wa kiusalama wa nchi zote lazima upewe uzito, na juhudi zote zinazofaa kwa utatuzi wa amani wa mgogoro lazima ziungwe mkono.

Kwa upande wa Macron na Scholz wameeleza mawazo na misimamo yao kuhusu hali ya Ukraine wakisema kwamba Ulaya inakabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia, na Ufaransa na Ujerumani wanaunga mkono kutatua mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo, na kuipatia nafasi amani.