Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lafanya mkutano wa pili katika kikao cha mwaka
2022-03-08 08:54:44| CRI

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), likiwa ni chombo cha ngazi ya juu cha kutoa ushauri wa kisiasa nchini China, jana Jumatatu lilifanya mkutano wa pili katika kikao chake cha mwaka.

Bw. Wang Yang, mjumbe wa kamati ya kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati ya taifa ya baraza hilo, alihudhuria mkutano huo. Wajumbe 12 wa kamati ya taifa ya baraza hilo walitoa maoni yao kwenye mkutano huo.

Bw. Ge Huijun, ambaye ni mmoja wa wajumbe hao, alitoa wito kwa washauri wa kisiasa kubeba majukumu yao na kutekeleza kwa moyo wote demokrasia ya kisoshalisti ya kushauriana.