Rais Xi Jinping asisitiza kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria
2022-03-08 08:50:40| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria na kuhimiza utawala wa sheria kwenye ulinzi wa taifa na ujenzi wa jeshi.

Rais Xi amesisitiza hayo alipokutana na wajumbe wa jeshi la ukombozi wa umma na wa jeshi la polisi, kwenye kikao cha tano cha mkutano wa 13 wa bunge la umma la China unaoendelea mjini Beijing. Rais Xi amepongeza mafanikio yaliyopatikana kwenye usimamizi wa jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya juhudi za miaka mingi toka mwaka 2012 ulipofanyika mkutano mkuu wa Chama cha kikomunisti cha China.

Rais Xi amesema kwenye kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria, mkazo unatakiwa kuwekwa kwenye kuunda jeshi la kimapinduzi, la kisasa na lenye vigezo, na kujenga mfumo wa China wa kusimamia mambo ya jeshi kwa mujibu wa sheria.