Ofisa wa UM aeleza wasiwasi juu ya kuuawa kwa watu wenye asili ya Afrika na polisi nchini Marekani
2022-03-09 08:41:14| CRI

Ofisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema idadi kubwa ya watu wenye asili ya Afrika wanauawa na watekelezaji wa sheria katika nchi nyingi, haswa nchini Marekani.

Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, amesema kwenye ripoti yake ya kila mwaka iliyowasilishwa kwenye kikao kinachoendelea cha 49 cha Baraza la Haki za Binadamu kwamba nchini Marekani, asasi za kiraia zimerekodi mauaji ya watu 266 wenye asili ya Afrika yaliyofanywa na polisi mwaka 2021.

Bibi Bachelet amezihimiza mamlaka za kitaifa katika sehemu zote duniani kuhakikisha watekelezaji wa sheria wanaohusika na mauaji kama hayo wanawajibishwa kwa haraka na kwa ufanisi.