Mashirika ya ndege ya Ethiopia na Djibouti yashirikiana katika usafirishaji kwa njia ya bahari na anga kati ya China na Afrika
2022-03-09 09:13:03| CRI

Shirika la ndege la Ethiopia ET limetangaza kushirikiana na shirika la ndege la Djibouti na Eneo la viwanda la Djibouti IDIPO kufanya usafirishaji kwa njia ya bahari na anga.

Shirika hilo limetoa taarifa ikisema, makubaliano hayo yatatafuta kusafirisha mizigo kutoka China hadi eneo huria la Djibouti kwa njia ya bahari na kuisafirisha tena kwa ndege kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Djibouti.

Shirika hilo limedokeza kuwa ushirikiano huo wa pande mbili utakaopunguza muda na matumizi ya nishati katika ugavi, utahimiza ukuaji wa soko la uchukuzi wa mizigo barani Afrika.

Shirika hilo pia limesema makubaliano hayo yatawawezesha wafanyabiashara kuagiza bidhaa zao kutoka China hadi Afrika kupitia bandari ya Djibouti, na shirika hilo litapeleka bidhaa hizo katika sehemu tofauti za Afrika kupitia mtandao wake wa ndege.