Bunge la umma la China lafanya kikao cha pili cha wajumbe wote
2022-03-09 09:04:03| CRI

Bunge la 13 la umma la China, jana lilifanya kikao cha pili katika mkutano wake wa tano wa mwaka kilichohudhuriwa na viongozi waandamizi wa China wakiwemo Rais Xi Jinping na Waziri Mkuu Bw. Li Keqiang.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Bw. Li Zhanshu, aliwasilisha ripoti ya kazi ya kamati kwenye kikao hicho, akieleza jinsi kamati ilivyoboresha sheria zinazohusu katiba na kuimarisha hadhi yake ya kisheria, madaraka yake na nguvu yake. Amesema kamati pia imeimarisha usimamizi mkali na wenye ufanisi, na kutoa uungaji mkono na ulinzi kwa wajumbe wa bunge la umma kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Kwenye kikao hicho wajumbe wa bunge la umma pia walisikiliza ripoti ya kazi ya mahakama kuu ya umma iliyotolewa na mkuu wa mahakama hiyo Bw. Zhou Qiang. Bw. Zhou amesema katika mwaka uliopita, mahakama kuu ilifanya kazi kuhusu ulinzi wa taifa na utulivu wa jamii, kuhudumia maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuendelea kutoa kipaumbele kwa watu kwenye utendaji wake, na kuhimiza mageuzi ya mfumo wa sheria.