Rais Joe Biden atangaza vikwazo vya nishati dhidi ya Russia
2022-03-09 09:03:31| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza vikwazo vya nishati dhidi ya Russia, na kupiga marufuku uagizaji wa mafuta, gesi na makaa ya mawe kutoka Russia kutokana na kuendelea kwa operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine.

Akiongea kwenye ikulu ya Marekani Rais Biden amesema hii ina maana kuwa mafuta kutoka Russia hayatakaribishwa kwenye bandari za Marekani, hatua ambayo ameitaja kuwa itakuwa pigo kubwa kwa uwezo wa Russia kugharamia operesheni zake za kijeshi. Hata hiyo amekiri kuwa hatua hiyo inaweza kuwaathiri wamarekani kwa kufanya bei za mafuta zipande.

Bei ya mafuta nchini Marekani imeongezeka kwa asilimia 15 na kuwa zaidi ya dola 4 kwa galoni moja. Na Umoja wa Ulaya ambao asilimia 40 ya gesi yake inaagizwa kutoka Russia, umetangaza hatua za kupunguza uagizaji wa gesi kutoka Russia, na hatimaye kuacha kabisa kuagiza kuanzia mwaka 2030.