China yatoa shehena ya tatu ya chanjo ya COVID-19 kwa UNRWA
2022-03-10 09:29:15| CRI

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limetoa taarifa kuwa limepokea shehena ya tatu ya chanjo ya COVID-19 kutoka China.

Chanjo hiyo imewasilishwa kwenye matawi matatu ya UNRWA, yakiwemo Jordan, Lebanon na Syria, ambazo zinaesaidia kuwahifadhi wakimbizi wa Palestina na kutoa mchango katika mpango wa utoaji chanjo katika nchi hizo.

Mkuu wa Ofisi ya China nchini Palestina Bw. Guo Wei, ameshukuru utoaji endelevu wa misaada na huduma muhimu wa UNRWA kwa wakimbizi wa Palestina, akisema China itaunga mkono kazi za shirika hilo na kuendelea kutoa misaada halisi kwa wakimbizi wa Palestina.