Rosa Mistika Riwaya ya Euphrase Kezilahabi ni kitabu chenye kujenga taswira fika ya maisha na malezi ya mtoto wa kike kwa Jina Rosa Mistika na changamoto anazozipata katika jamii kutokana na malezi yenyewe, tamaduni, umaskini na mateso ya kifamilia. Pia kinaangazia kutawishwa kwa watoto wa kike na athari zake. Wapo wanaomwita malaya, mzinzi mkuu, mvunja nyumba za watu; na wapo wengine wanaomwona kama msichana mwenye nafsi isiyo na hatia, msichana aliyekuwa amezingwa na kutekwa nyara na shinikizo hasi za mazingira, yakamghilibu bila ya kujitambua.