Msomi wa Tanzania: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yatoa faraja kwa dunia inayosumbuliwa na janga la Corona
2022-03-10 10:56:03| CRI

Msomi wa Tanzania: Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yatoa faraja kwa dunia inayosumbuliwa na janga la Corona_fororder_VCG111164870804

Natumaini u mzima buheri wa afya msikilizaji na unaitegea sikio CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing. Karibu katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu, na ni kipindi ambacho kimesheheni mambo mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, na jinsi urafiki, ushirikiano na uhusiano kati ya pande hizo unavyozisaidia kupata maendeleo ya pamoja.

katika kipindi cha leo ripoti yetu itahusu Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing ambayo ilianza wiki iliyopita, na pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yatakayozungumzia kampuni ya China kuzindua paneli yake ya umeme wa jua nchini Kenya.