Tanzania yachukua tahadhari ya juu kufuatia mlipuko wa homa ya manjano kuripotiwa Kenya
2022-03-10 09:04:16| CRI

Mamlaka ya afya nchini Tanzania imesema serikali iko katika tahadhari ya juu kufuatia mlipuko wa homa ya manjano kuripotiwa katika nchi jirani Kenya.

Waziri wa Afya wa Tanzania Bibi Ummy Mwalimu amesema wizara yake imeimarisha ukaguzi dhidi ya virusi hivyo kwenye mipaka na vituo vingine vya forodha zikiwemo bandari na viwanja vya ndege.

Bibi Mwalimu amewaambia wanahabari mjini Dodoma kuwa wasafiri kutoka nchi zenye hatari kubwa katika bara la Afrika na Latin Amerika hawaruhusiwi kuingia nchini bila cheti cha chanjo ya homa ya manjano.

Waziri huyo amesema Tanzania haijashuhudia mlipuko wowote wa homa ya manjano tangu mwaka 1950.