Jeshi la China lashirikiana na majeshi ya nchi zaidi ya 50 kupambana na janga la Corona
2022-03-10 09:23:19| CRI

Msemaji wa Jeshi la ukombozi wa Umma la China PLA amesema jeshi hilo limetoa mchango mkubwa katika mapambano ya kimataifa dhidi ya janga la COVID-19, huku likiunga mkono kikamilifu udhibiti wa maambukizi ndani ya nchi.

Msemaji wa ujumbe wa Jeshi la PLA na Kikosi cha Polisi Bw. Wu Qian, anayehudhuria mkutano wa tano wa bunge la 13 la umma la China, amesema jeshi la China limetoa msaada wa chanjo kwa majeshi ya nchi zaidi ya 20 zikiwemo Pakistan, Cambodia, Mongolia na Guinea ya Ikweta.

Amesema jeshi hilo limeanzisha ushirikiano na majeshi ya nchi zaidi ya 50 katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa kutoa vifaa tiba, kutuma timu za wataalamu wa afya, na kufanya mikutano kwa njia ya video kubadilishana uzoefu.