Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa
2022-03-10 11:58:10| CRI

Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa_fororder_1128416470_1646882311899_title0h

Mkutano wa 5 wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China umefungwa baada ya kumaliza ajenda mbalimbali kwa mafanikio.

Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China akiwemo rais Xi Jinping wamehudhuria hafla ya kufungwa kwa mkutano huo.

Mkutano huo umepitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya Baraza hilo, azimio kuhusu utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa tangu Mkutano wa 4 wa Baraza hilo, ripoti ya uchunguzi wa mapendekezo hayo, na azimio la kisiasa kuhusu mkutano huo.