Wajumbe wa Mikutano Miwili wazingatia kulinda haki na maslahi za wanawake
2022-03-11 09:00:43| Cri

Hivi sasa mikutano miwili inayofuatiliwa sana inaendelea mjini Beijing, huku ulinzi wa haki na maslahi ya wanawake unaendelea kuwekwa mkazo mkubwa. Haki na maslahi ya wanawake ni suala linalozingatiwa wakati wa Mikutano Miwili kila mwaka, lakini kwa mwaka huu linafuatiliwa zaidi katika mikutano hiyo. Sababu ni kwamba kuanzia mwishoni mwa mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu, Rasimu ya Marekebisho ya Sheria ya Kulinda Haki na Maslahi ya Wanawake ilikusanya maoni ya umma, na watu zaidi ya elfu 80 walitoa jumla ya maoni zaidi ya laki 4.2.