Mkutano wa 5 wa Bunge la 13 la Umma la China wafungwa
2022-03-11 11:07:08| CRI

Mkutano wa 5 wa Bunge la 13 la Umma la China wafungwa_fororder_VCG111372741629

Mkutano wa 5 wa Bunge la 13 la Umma la China umefungwa baada ya kumaliza ajenda mbalimbali. Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China akiwemo Rais Xi Jinping wamehudhuria hafla ya kufungwa kwa mkutano huo.

Spika wa Bunge hilo Li Zhanshu amesema huu ni mwaka muhimu wa mchakato wa maendeleo ya shughuli za Chama cha Kikomunisti cha China na taifa la China, inapaswa kutekeleza kwa kina msingi wa Mkutano wa serikali kuu kuhusu kazi za Bunge la Umma, kutambua kwa kina majukumu mapya ya Bunge hilo katika mfumo wa utawala, na kuinua kiwango cha Bunge hilo.