China haitafunga mlango wake
2022-03-11 15:04:28| CRI

China haitafunga mlango wake_fororder_1128460170_16469698047821n

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo amesema China imetekeleza sera ya kufungua mlango kwa zaidi ya miaka 40, sera ambayo imeleta maendeleo kwa China na manufaa kwa dunia nzima, kwa hiyo China haitafunga mlango wake.
Bw. Li ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mkutano wa 5 wa Bunge la 13 la Umma la China. Amesema China imejiunga na uchumi wa dunia, itaendelea kusukuma mbele biashara huria, na kuifanya China iwe nchi inayovutia zaidi uwekezaji kutoka nje.
Bw. Li pia amesema, serikali ya China siku zote inapaswa kulenga kuhakikisha na kuboresha maisha ya watu inapoendeleza uchumi. Amesema katika miaka mingi iliyopita, mapato ya watu yameongezeka sambamba na ukuaji wa pato la taifa la China, lakini China bado ni nchi inayoendelea, na kuna pengo dhahiri kati ya miji na vijiji, kuzifanya huduma za kiumma ziwe na usawa, huu ni mchakato wa muda mrefu. Ameongeza kuwa China itaongeza bajeti ya elimu ya lazima vijijini na sehemu zilizoko mbali.